
Kulingana na kanuni za kitabu kinachouzwa sana nchini Marekani When Helping Hurts: How to Alleviate Poverty without Hurting the Poor… and Yourself (Moody Publishers, 2009, 2012)
Kusaidia Bila Kuumiza Barani Afrika kinawapa wasomaji misingi na zana muhimu za kuondoa umaskini kwa mtazamo wa Kristo, na pia kinatumika kama mwongozo wa mwalimu unaoweza kutumika moja kwa moja kusaidia washiriki:
- Kukua katika uhusiano wao na Mungu, wengine, nafsi zao, na viumbe vingine vyote.
- Kupata mtazamo mpya kuhusu ufalme wa Mungu katika huduma zao.
- Kufufua upendo na huruma yao kwa maskini wa kimwili.
- Kupata maarifa kuhusu jinsi ya kuwasaidia watu na jamii zenye kipato cha chini kwa hekima zaidi.
- Kuwezesha makanisa na huduma kuleta mabadiliko ya kudumu, kuanzia na rasilimali walizo nazo.
Jonny Kabiswa Kyazze ni raia wa Uganda mwenye Shahada ya Uzamili katika Usimamizi na Maendeleo ya Mashirika, Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika Maendeleo Yanayotegemea Jamii, na Stashahada ya Usimamizi wa Biashara. Amefanya kazi katika mashirika mbalimbali ya kimataifa ya maendeleo katika ngazi tofauti za usimamizi na ana uzoefu wa zaidi ya miaka 16 katika maendeleo yanayotegemea jamii. Jonny pia ni mshauri katika usimamizi na maendeleo ya mashirika na mwandishi wa kitabu Influence of Organizational Culture on Employee Performance.
Anthony Sytsma na mkewe, Sara, wanahudumu katika shirika la Resonate Global Mission nchini Uganda, ambapo Anthony huwalea na kufundisha wachungaji. Ana shauku ya kuwahimiza Wakristo wa Marekani kusikiliza na kujifunza kutoka kwa Wakristo wa Afrika ili waweze kushirikiana katika kubadilisha mbinu za kimisioni na maendeleo barani Afrika. Anthony anatoka jimbo la Michigan, Marekani, na ana Shahada ya Kwanza ya Sanaa katika Dini na Theolojia kutoka Chuo Kikuu cha Calvin na Shahada ya Uzamili ya Uungu kutoka Chuo cha Theolojia cha Calvin.
Dkt. Brian Fikkert ni Mwanzilishi na Rais wa Chalmers Center for Economic Development katika Covenant College, ambako pia ni Profesa wa Uchumi na Maendeleo ya Jamii. Yeye ni mwandishi mwenza wa vitabu nane, kikiwemo kile kinachouzwa sana When Helping Hurts: How to Alleviate Poverty Without Hurting the Poor… and Yourself. Dkt. Fikkert alipata Shahada yake ya Uzamivu (Ph.D.) katika Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Yale, akibobea katika uchumi wa kimataifa na maendeleo ya kiuchumi.
“Kujifunza kuhusu aina nne za umaskini kumenisaidia kuelewa maana ya kuwasaidia watu wengine.”
–Mchungaji Rogers Mumba, Zambia










Share on Social Media
Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn